Muharram - Arusha - 1447H / 2025 Matembezi ya Amani ya A'shura - Jijini Arusha - Tanzania katika Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hussein (a.s) yalifanyika Jana Tarehe 06-07-2025 yakibeba kauli Mbiu: "KARBALA, SIRI YA USHINDI WETU"

7 Julai 2025 - 23:29

Matembezi ya Amani ya kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hussein (as) yamefanyika kwa mafanikio makubwa Jijini Arusha- Tanzania + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Matembezi ya Amani ya kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hussein (as) yamefanyika kwa mafanikio makubwa Jijini Arusha- Tanzania yakiambatana na Kauli Mbiu: Karbala ni Siri ya Ushindi wetu.

Matembezi ya Amani ya kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hussein (as) yamefanyika kwa mafanikio makubwa Jijini Arusha- Tanzania + Picha

Ufafanuzi wa Kauli hii:

"Karbala ni siri ya ushindi wetu

Hii ni kauli mbiu iliyotumika katika Matembezi ya Amani ya Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (as) Jijini Arusha, ambayo inaangazia umuhimu wa matukio ya Karbala katika historia ya Kiislamu, hasa kwa Waislamu wafuasi wa Ahlul-Bayt (as). 

Vita vya Karbala, ambapo Imam Hussein(as), Mjukuu wa Mtume Muhammad(saww), alipigana dhidi ya jeshi la Muovu Yazid bin Muawia (L.A), ulimwengu wa Kiislamu unavitambua kama ishara ya ujasiri, imani, na kujitolea kwa ajili ya Kuitetea Haki , Ukweli na Uadilifu.

Katika muktadha huu, "Ushindi" haumaanishi tu kushinda vita, bali pia unajumuisha ushindi wa kiroho na kimaadili. 

Karbala inawakilisha mapambano dhidi ya udhalimu na uonevu, na inatoa mafunzo muhimu kuhusu umuhimu wa kusimama kwa ajili ya haki na imani, hata licha uwepo wa vikwazo vikubwa.

Kauli mbiu hii ni muhimu mno kwa sababu imetumika ikilenga kuhamasisha watu kuiga mfano wa Imam Hussein(as) na kupigania haki na usawa katika jamii zao.

Your Comment

You are replying to: .
captcha